Saturday, August 10, 2024

Field Officers (5 Posts) at Mbarali Estates Ltd August 2024

  AjiraLeo Tanzania       Saturday, August 10, 2024
Mbarali Estates Limited
Jobs in Tanzania 2024: New Job Vacancies at Mbarali Estates Limited 2024

💥UNASUBIRI NINI? FOLLOW US ON INSTAGRAM. CLICK HERE!💥

Mbarali Estates Limited Jobs 2024

BWANA SHAMBA WA MAHINDI (FIELD OFFICER)
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI.
Nafasi : Bwana shamba wa Mahindi - Nafasi 5 katika Kampuni ya Highland Estates Limited - Mbarali
Kampuni ya Highland Estates Limited – Mbarali iliyopo katika Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Mbarali inayojishughulisha na Kilimo cha Umwagiliaji na Ufugaji inatangaza nafasi za ajira ya Bwana Shamba mwenye ujuzi, uzoefu na utaalamu husika katika Shamba lake la Mahindi.

MAJUKUMU YA BWANA SHAMBA WA MAHINDI (FIELD OFFICER)
1. Kusimamia shughuli zote za uzalishaji katika msimu kwa kuzingatia kalenda.
2. Kuandaa na kusimamia programu ya kuandaa Shamba pamoja na kulima kwa wakati.
3. Kuandaa kalenda ya umwagiliaji (Irrigation scheduling) kwa Shamba la Mahindi
4. Kuhakikisha Shamba la Kampuni Linapandwa ndani ya Msimu Husika na kuandaa Kalenda ya Msimu wa Kupanda na Kuvuna.
5. Kuandaa mpango kazi na kusimamia ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji katika Shamba.
6. Kuandaa na kusimamia matumizi bora ya zana za kilimo.
7. Kuhakiki na kusimamia matumizi ya mbolea na viuatilifu
8. Kusimamia na Kuratibu maswala ya mazingira katika Shamba.
9. Kuandaa ripoti ya mwezi, robo, nusu, robo tatu mwaka na mwaka mzima.
10. Kushirikiana na Kampuni katika kuandaa mipango ya maendeleo ya muda mfupi na ya muda mrefu.
11. Kuandaa taarifa ya matumizi ya Madawa, Mbolea pamoja na Viuatilifu kwa msimu mzima
12. Kuajiri vibarua na kuwasimamia katika shughuli za uendeshaji shambani.
13. Kushirikiana na wafanyakazi wengine wa kampuni katika kutimiza malengo mapana na makubwa ya kampuni.
14. Kufanya kazi nyingine atakazoelekezwa na kiongozi wako.
15. Kufanya kazi nyingine utakazopangiwa na Mwajiri wako bila kuathiri ujuzi/elimu uliyonayo
i. Awe raia wa Tanzania.
ii. Awe na Astashahada au Shahada ya Kilimo kutoka katika chuo kinachotambulika na Serikali ya Jamhuri yo Muungano wa Tanzania.
iii. Awe na Ujuzi wa kutumia kompyuta.
iv. Asiwe na rekodi ya kushitakiwa kwa kosa la jinai ama rushwa.
v. Awe mwenye umri kati ya 25 – 35.
vi. Awe na wezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea katika hali yeyote.
vii. Uzoefu wa mwaka 3.
viii. Anayejua lugha ya Kiingereza na Kiswahili fasaha.

Ø MSHAHARA: Maelewano

Ø NAMNA YA KUTUMA MAOMBI.
Waombaji wote lazima wawe Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 35.
Watu wenye sifa zinazofaa wanapaswa kutuma maombi yao kwa barua pepe ya erickrutakyamirwa@gmail.com wakiambatanisha nakala za vyeti vyao vya kitaaluma pamoja na Wasifu (CV), Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30/08/2024.
Namna ya kutuma maombi
Maombi yatumwe kwa:-
Afisa Utumishi,
Highland Estates Limited - Mbarali
P.O Box 78 Rujewa
Mbeya, Tanzania
.
logoblog

Thanks for reading Field Officers (5 Posts) at Mbarali Estates Ltd August 2024

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment